The House of Favourite Newspapers

ROMA AMUANIKA MWANAYE

BAADA ya kumficha kwa kipindi cha miezi sita, hatimaye staa wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Musa ‘Roma Mkatoliki’ ameamua kumuanika mwanaye wa kike, Ivy. Ishu hiyo imetokea juzikati, baada ya Star Showbiz kumtimbia nyumbani kwake, Mbezi- Jogoo jijini Dar ambapo alikuwa akifanya sherehe ya kumbatiza mtoto huyo.

“Nimekuwa siyo mtu wa kuanika anika hovyo maisha yangu na wanangu lakini kwa kuwa umetokea haina jinsi, huyu hapa ni Ivy, leo ndiyo amebatizwa rasmi,” alisema Roma akionesha picha zake nyingine.

Roma anayebamba na Ngoma ya Parapanda akiwa na Stamina, anaishi na mkewe wa ndoa, Nancy ‘mama Ivan’ na wamebahatika kupata watoto wawili, Ivan na Ivy.

Comments are closed.