The House of Favourite Newspapers

Chadema Yatoa Tamko Zito, Yataka Kukamilika kwa Katiba Mpya Kabla ya 2025

0
Katibu Mku wa Chadema John Mnyika

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kupitia kwa Katibu Mkuu wake John Mnyika kimetoa taarifa juu ya mazungumzo ambayo Cham hicho kilifanya hivi karibuni na Ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

 

Akiongea na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Chama hicho, Mnyika amesema kuwa Ujumbe wa CHADEMA ulienda na ajenda kuu mbili ambazo ndani ya ajenda hizo ulikuwa na mambo kadha wa kadha ya kujadili na kuona utekelezaji wake ukikamilika kwa manufaa ya wanachama wa CHADEMA nan chi kwa ujumla.

 

Mnyika amesema Ujumbe wa CHADEMA uliwasilisha ajenda mbili ambazo ni kurejeshwa na kukamilika kwa mchakato wa Katiba mpya nchini na ajenda ya pili ilikuwa ni kutatua madhara yaliyotokana na ukiukwaji wa Katiba katika kipindi cha Utawala wa Awamu ya Sita.

 

Katibu Mkuu huyo ametoa rai kwa wanachama wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kuwa watulivu kwani lengo la Chama hicho ni kuhakikisha ajenda hizo zinashughulikiwa lakini pia zinakamilika ndani ya muda kabla ya kufikia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Leave A Reply