The House of Favourite Newspapers

Chalamila Mkuu Mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Achukua Nafasi ya Amos Makalla

0

Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa wanne ambapo amemhamishia jijini Dar es Salaam, Albert Chalamila aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Chalamila anachukua nafasi ya Amos Makalla aliyehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza huku aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwassa akihamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, akichukua nafasi ya Chalamila.

Pia Rais Samia, amemhamisha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akichukua nafasi ya Fatma Mwassa aliyehamishiwa Kagera.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus leo Mei15, 2023 inaeleza kuwa uteuzi huo unaanza mara moja

Leave A Reply