The House of Favourite Newspapers

Chameleon, Nyashinski, King Kiba Unyama Mwingi, Wafunika Mbaya Serengeti Lite Oktoba Fest

0
King Kiba alivyokiwasha jukwaani.

Dar es Salaam 22 Oktoba 2023: Wasanii kutoka Afrika Mashariki, akiwemo Ali kiba, kutoka Tanzania, Nyashinski, kutoka Kenya na Jose Chameleon usiku wa kuamkia leo walifanya unyama mwingi na kulinogesha ile mbaya tamasha la Serengeti Lite Oktoba Fest lililofanyika Ufukwe wa Coco jijini Dar-es-Salaam.

Akizungumza  na wanahabari, wakati wa tamasha hilo Meneja Mahusiano na Uendelevu kutoka SBL, Rispa Hatibu amesema kuwa Oktoba Festival ni ya kwanza kabisa na kubwa kuwahi kutokea Tanzania na litafanyika nchi tatu za nchi za Afrika Mashariki ambazo ni hapa nchini, Kenya na Uganda.

Mashabiki wakiwa katika mayowe ya furaha.

Amesema kwa upande wa Uganda litafanyika kesho, Sudani Kusini litafanyika wiki ijayo na Kenya litafanyika mwisho wa mwezi.

“Niseme tu hili ni tamasha  ni kubwa ambalo halijawahi kutokea, kwetu ni mara ya kwanza  na litakuwa endelevu na kila mwaka tutaleta mambo mapya na makubwa  hapa Tanzania, Uganda na Sudani Kusini halijawahi kufanyika.

Kwa wenzetu Kenya litakuwa la mara ya tano ama sita hivyo basi ndio maana umeona leo wasanii wamefanya kile ambacho kilipaswa kufanyika ili kuleta burudani ambayo imemkonga kila mtu aliyefika eneo hili.

Mashabiki wakiangalia shoo huku wakiburudika na Serengeti Lite.

“Tulivyoilenga hii Oktoba Festival siyo tu kwenye burudani lakini pia kuna faida ambayo tumeileta kwenye uchumi, leo kuna wafanyabiashara wengi wamekuja kuuza na kuonyesha bidhaa zao ambazo wamepata fursa ya kuuza na kutangaza.

Upande wa mazingira kama mnavyoona mpaka asubuhi hakuna uchavuzi wa fukwe kwa sababu hatukuwa na plastiki tulikuwa na vikombe vya bati pamoja na vya karatasi ambayo havikuharibu mazingira na tulikuwa na vijana wengi ambao walikuwa wanatembea kila kona kukusanya uchafu na hivyo tumeacha mazingira yakiwa safi kabisa.” Amesema Rispa.

Miongoni mwa wasanii waliopiga shoo hiyo ni pamoja na Gnako, Billnass, Ali Kiba, Chino Wana man, Jose Chameleon na Nyashinski na wengineo kibao.

Leave A Reply