The House of Favourite Newspapers

Chamudata Mpya Yaanza Mikakati Kuinua Muziki wa Dansi

0
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chamudata, Rhobi Chacha akiwakaribisha wanahabari (hawapo pichani) kwenye mkutano huo. Kushoto ni katibu wa chama hicho, Saidi Kibiriti. 

 

 

VIONGOZI wapya wa Chama cha muziki wa dansi nchini, CHAMUDATA wameweka hadharani mikakati yao baada ya kuingia madarakani Mei 21 mwaka 2022.

 

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari Mwenyekiti wa CHAMUDATA Luiza Nyoni ambaye ni mwanamuziki mkongwe wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ alianza na kuwashukuru wapiga kura waliouingiza madarakani uongozi huo.

Mwenyekiti mpyta wa Chamudata, Luiza Nyoni akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni makamu wake Abdallah Hemba.

 

Luiza alianza na kuwatambulisha viongozi wenzake waliokuwa kwenye mkutano huo na kuanza na yeye mwenyewe, makamu wake, Abdalallah Hemba, Katibu, Saidi Kibiriti, wajumbe Rhobi Chacha, Sesi Jeremiah, Eddo Sanga na Said Mdoe.

 

Baada ya kuutambulisha uongozi huo Luiza alisema chama hicho kuanza sasa kitakuwa chini ya mwamvuli wa shirikisho la muziki na wajumbe wane kutoka chama hicho watakuwa mongoni mwa wajumbe wa bodi ya shirikisho hilo.

Mkutano ukiendelea.

 

Luiza aliendelea kusema;

“Uongozi wetu umeanza kazi rasmi Mei 21 mwaka huu ambapo tukikabidhiwa ofisi ingawa hali ya kiofisi haikuwa nzuri kwa maana haikuwa na vitendea kazi kama vile kompyuta, viti, meza na fenicha zingine za kukamilisha ofisi.

 

“Tulikabidhiwa nyaraka zilizokuwa zikitumika kwenye ofisi hiyo lakini zilikuwa na mapungufu mengi yaliyosababisha hata tushindwe kuzitumia.

Mnenguaji wa Bogoss Muzika, Queen Suzy kushoto na mpiga dram wa kujitegemea Martin Kibosho wakifuatilia mkutano huo.

 

 

“Tulifanya ukaguzi kwenye akunti za chama ambapo tulikuta akaunti mbili za chama ya NMB na CRDB ambapo tulikwenda kuzikagua tukianzia na ile ya NMB na kukuta haina salio na tulipokwenda ile ya CRDB tulikuta tayari ilishakufa kabisa”.

 

“Ofisi tumeikuta haina pesa kabisa na mpaka sasa tumeanza kazi kwa kuindesha kwa kutumia pesa zetu za mfukoni.” Alisema mwenyekiti Luiza na kuendelea.

 

“Baada ya kuona hivyo tukaona tufungue akaunti ili tuanze nayo lakini tukakuta chama hakina hata akaunti hivyo kushindwa kufungua akaunti kwa haraka na kuamua kusajili laini ya simu ndiyo tuanze kuingiza chochote kwa mhisani anayetaka kuanza kutusaidia” alisema Luiza.

 

Pamoja na changamoto zote hizo Luiza alieleza malengo yao kumi wanayotaka kuanza nayo ambapo ni pamoja na kutengezeza mfumo wa kuwasajili wanamuziki wote wa dansi, kulinda haki miliki na haki shiriki kwa wanamuziki, kuandaa tamasha kubwa litakalowakuwanisha wanamuziki wote, kuongeza wanachama nchi nzima na mengineyo.

 

Luiza aliwaambia wanahabari kuwa hivi karibuni baada ya kuchaguliwa uongozi wao walialikwa bungeni na kufanikiwa kukutana na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas ambaye aliwaahidi kuwatafuta na kukaa nao pamoja na wadau wengine ili kujadili kiupana malengo yao. Alimaliza kusema Luiza.

Leave A Reply