The House of Favourite Newspapers

Chanjo ya Minyoo, Matende na Mabusha Yazinduliwa Dar

0

1.Wauguzi wa Wilaya ya Kinondoni wakitoa dawa za chanjo kwa wakazi wa maeneo ya Manzese Dar.Wauguzi  mbalimbali wa Wilaya ya Kinondoni wakitoa dawa za chanjo kwa wakazi wa Manzese Dar.2.Mmoja wa akina mama akiwa kwenye mstari wa kuchukua vidonge vya kuzuia, ninyoo, matende na mabusha kwenye zahanati ya manzese.Mmoja wa akina mama akiwa kwenye mstari kuchukua vidonge vya kuzuia minyoo, matende na mabusha kwenye Zahanati ya Manzese.3.,Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dkt. Azizi Msuya (kulia) akimnywesha dawa mtoto aliyefika kwenye zahanati ya Manzese kwa ajili ya kinga ya chanjo ya minyoo,matende na mabusha.Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dkt. Azizi Msuya (kushoto) akimnywesha dawa mtoto aliyefika kwenye Zahanati ya Manzese kwa ajili ya chanjo hiyo.4.Dkt. Azizi Msuya akihojiwa na wanahabari kwenye uzinduzi huo wa chanjo.Dkt. Azizi Msuya akihojiwa na wanahabari kwenye uzinduzi wa chanjo hiyo.5.Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Manzese, Nestory Kobero akihojiwa na mwanahabari.Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Manzese, Nestory Kobero akihojiwa na mwanahabari.

CHANJO ya minyoo, matende na mabusha imezinduliwa leo katika  Zahanati ya Manzese, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar ambapo wakazi wa maeneo hayo wameonekana wakiunga mkono uzinduzi huo.

Akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi huo, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dkt. Azizi Msuya amesema wananchi  wanapaswa kufika kwenye vituo vya afya na zahanati kwa ajili ya kupata chanjo ya kuweza kujikinga na magonjwa hayo.

Amesema kuwa chanjo hiyo haina madhara yoyote na  hutolewa bure bila malipo hivyo sasa ni wajibu  wananchi kujitokeza kupata chanjo hiyo ya kuzuia magonjwa kutokuendelea katika jamii.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply