The House of Favourite Newspapers

Chanzo cha Kifo cha Prodigy Chafanywa Siri

0

Mwanamuziki nchini Marekani ambaye pia ni rais wa Kundi la Mobb    Deep,  Albert Johnson maarufu kwa jina la Prodigy amefariki dunia siku ya Jumanne, Juni 20, 2017 akiwa na umri wa miaka 42 na mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado haijawekwa wazi.

Taarifa ya kifo chake imetumwa kwenye tovuti ya muziki ya XXL na msemaji wa kundi hilo la Muziki wa Hip Hop linalofanya vizuri nchini Marekani ambapo baada ya Prodigy kufariki limebaki na wasanii wawili tu Havoc na Big Noyd.

Prodigy alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kurithi ya Anemia ugonjwa ambao husababisha uzuiaji mbaya wa mtiririko wa damu. Mara ya mwisho alikuwa katika ziara jijini Las Vegas, Nevada akifanya sanaa ya Rap na ndipo mauti yalipomkutia.

Kundi la Mobb Deep lililokuwa likiongozwa na Prodigy limewahi kuandika historia katika muziki nchini Marekani baada ya kuchapisha na kuuza nakala zaidi ya milioni tatu za Albamu ya Jehanamu na likapata mafanikio makubwa miaka ya 1990 na mwaka 2014 lilitoa albamu yao ya nane inayoitwa Infamous Mobb Deep

Na Isri Mohamedi

Leave A Reply