The House of Favourite Newspapers

Cheki Kanye West alivyomuokoa Paparazi

0

kanye-west-lax

IKIWA imepita miaka mitatu tangu rapa Kanye West ‘Yeezy’ azinguane na paparazi ‘live’ juzikati amewashangaza watu baada ya kuonekana tena katika tukio linalohusisha mapaparazi.

Ijumaa iliyopita, Yeezy alikuwepo katika Jiji la Los Angeles, Marekani ambapo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari akifanyiwa mahojiano kuhusiana na Albamu yake mpya ya The Life Of Pablo (T.L.O.P).

Akiwa katika kujibu maswali ghafla paparazi mmoja akamsukuma mwenzake na kuzuka ugomvi mkubwa ambao Yeezy aliingilia kati na kumkumbatia mmoja wapo ili wasiendelee kugombana.

Baada ya kuuzuia ugomvi huo, Kanye alirejea kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na wapiga picha kuhusiana na kuendelea kutafuta mtoto wa tatu akajibu labda “Perhaps” na alipoulizwa kama Mark Zuckerberg atampa pesa akajibu “He might end up helping out. 

https://youtu.be/Y4uzi7KzV-k

Video 

Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

Leave A Reply