The House of Favourite Newspapers

Chelsea Yaifanyia Umafia Real Madrid na PSG Usajili wa Kinda wa Brazil

0
Endrick Felipe Kinda wa Brazil anayewatoa udenda Chelsea, Real Madrid na PSG

KLABU ya Chelsea ya nchini Uingereza imefanya umafia mkubwa dhidi ya vilabu vya Real Madrid na PSG kwenye usajili wa kinda wa Brazil kutoka klabu ya Palmeiras, Endrick.

 

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 16 anatajwa kuwa moja kati ya nyota vijana wanaotazamiwa kuja kuwa tishio kubwa katika ramani ya soka duniani huku vilabu vikubwa barani ulaya vikipigana vikumbo kuwania Saini yake.

Endrick Felipe pamoja na familia yake wametembelea viwanja vya mazoezi pamoja na Uwanja wa Stamford Bridge

Taarifa zilizothibitishwa na Gazeti la The Times la nchini Uingereza zimebainisha kuwa Chelsea imefanya mazungumzo na mchezaji huyo pamoja na familia yake ikiwa ni sambamba na kuwapa mwaliko wa kutembea Uwanja wa Stamford Bridge pamoja na viunga vyake vya Cobham.

 

Katika tukio hilo Endrick anaripotiwa kutumia muda mwingi kufanya mazungumzo na Thiago Silva ambaye pia ni mchezaji kutoka nchini Brazil ambaye anawakilishwa na Kampuni ya Uwakala wa wachezaji ambayo pia inamsimamia Vinicius Jr wa Real Madrid aliyejiu ng ana klabu hiyo mwaka 2018 akitokea klabu ya Flamengo ya nchini humo.

 

Endrick anaruhusiwa kusaini mkataba na klabu yoyote barani Ulaya kuanzia mapema mwaka 2023 ambao utamruhusu kujiunga na klabu yake mpya mapema mwaka 2024 baada ya kuwa ametimiza umri wa maika 18.

Leave A Reply