The House of Favourite Newspapers

Chid Benz Adakwa na ‘Unga’

NGULI WA wa Hip Hop nchini Rashid Makwiro ‘Chid Benz anashikiliwa tena  na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya na hii inakuwa mara ya tatu kwa msanii huyu kukumbwa na sakata hili.

Akithibitisha taarifa hizo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP, Giless Muroto alisema kwamba ni kweli msanii huyo alikamatwa na taarifa kamili zitatolewa.

Kamanda Muroto alisema;

Ni kweli Chidi Benz mnamo Desemba 30, 2017, tulimkamata akiwa yeye na mke wake na vijana wawili. Tumemkamata akiwa na dawa za kulevya zidhaniwayo kuwa ni Heroine. jalada lake lipo tayari kwa Mwanasheria wa wa serikali linafanyiwa uchunguzi na muda wowote watapelekwa mahakamani

Aidha ameongza kuwa watuhumiwa wote bado wako mahabusu.

Comments are closed.