The House of Favourite Newspapers

Chid Benz, Mr. Blue, Mobeto Uso kwa Uso Dar Live

Bongo Fleva, Hamisa Mobeto

PATA picha kwa mara ya kwanza jukwaani unamuona msanii mpya wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto pembeni yake Chid Benz na Mr. Blue unajua nini kitatokea? Kama hujajua basi sogea ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar katika Sikukuu ya Eid al Hajj (Agosti 12) utajionea.

 

Iko hivi; wakali hao kwa mpigo wakiongezewa na Easy Man, Mzee wa Bwax watashusha shoo ya nguvu wakipigiwa matarumbeta na Kiroboto OG, kifupi jukwaa litachafuka!

 

Akizungumza na Risasi Vibes,Mratibu wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP Mjomba’ alisema tamasha hilo limepewa jina la Bonsi Vibe likimaanisha Usiku wa Bongo Fleva na Singeli.

Chid Benz

Unaachaje kuja kwa mfano? “Litakuwa tamasha la aina yake kwani Mobeto kwa mara ya kwanza atashuka katika Viwanja vya Dar Live na kupafomu ngoma zake zote kali kuanzia My Love, Tunaendana na Sawa.

 

Siku hiyo warembo wote, mashabiki, wanamitindo na wadau wa muziki watahamia Dar Live sijui wewe utakuwa upande gani,” alisema KP. Tamasha zima litakuwa kwa kiingilio kiduchu kuliko unavyodhania kwani kwa buku tano tu yaani 5,000 utapata burudani zote hizo.

Comments are closed.