The House of Favourite Newspapers

Chid Benz: Nimefanya Ngoma Mpya na Tupac, Namshusha Bongo Soon

0
Chidi Benz.

RAPA mkali wa ngoma Dar es Salaam Stand Up, Chidi Benz amezua jipya baada ya kudai kuwa aliyekuwa Rapa wa Marekani Marehemu Tupac Amaru Shakur ‘2Pac’, yuko hai na anaishi nchini Cuba, na kuongeza kwamba wanaongea kila siku kwa simu huku akieleza tayari ameshafanya naye ngoma itakayotoka hivi karibuni.

Chidi Benz ambaye kwa sasa anazungumzwa kwa skendo za utumiaji wa madawa ya kulevya, akiongea na eNewz ya EATV, alisema kuwa;

“Maneno yanayoongelewa kwamba 2Pac amefariki siyo kweli, kila siku ninaongea na 2Pac na hata sasa hivi nimetoka kuongea naye”

Mimi na 2Pac tumekutana Cuba, na tumefanya nyimbo ya pamoja, Mungu akisaidia hivi karibuni tutaachia nyimbo hiyo”.

“2Pac ana mpango wa kurudi kwenye game ya muziki, na wimbo wetu tuliorekodi ndiyo utamrudisha. Hivi karibuni 2Pac atakuja Bongo, ila atakuja kimya kimya kama alivyokuja Beckam,” aliongeza Chidi Benz.

2Pac enzi za uhai wake.

Pia Chid aliendelea kwa kusema;

“Baada ya kukutana na 2Pac tuliamua kurekodi baadhi ya vipande vya video ambavyo tutaanza kuvisambaza kwanza ili kuweza kuwajulisha watu kuwa 2Pac bado yupo hai na kuwaondoa watu fikra za kuwa 2Pac ni marehemu”.

Hata hivyo kitu cha kushangaza zaidi ni baada ya Chid kuendelea kusema kwamba anamdai 2Pac kipini chake cha puuani ambacho alimuazima walipokuwa wote nchini Cuba. 

Kama ilivyokuwa kwa Young Dee, Chid Benz naye ameonekana kuwa na hali ya kujichanganya sana katika maelezo yake kila anapoongea. 

Hivi karibuni Ali Kiba akiongea na eNewz alishauri serikali iingilie kati suala la Chid Benz na kumpatia matibabu. Na hata kama akibainika anajihusisha na madawa Alikiba alishauri

“Chid asifungwe bali apelekwe ‘rehab’ akatibiwe kwani kumfunga mtu anayetumia madawa ni kumtesa tu”.

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

===

Global TV Kenya: Cheki Polisi Walivyomnasa Jambazi Huyu

Sikiliza Hadithi za Mtunzi Eric Shigongo Hapa

Mawakili Kanda ya Ziwa Waliamsha Dude kwa Lissu

Leave A Reply