The House of Favourite Newspapers

CHIKOKA: TUSOME ALAMA ZA NYAKATI

MUIGIZAJI mkongwe wa sinema za Kibongo, Juma Chikoka ‘Chopa’ amewataka waigizaji wenzake pamoja na jamii kwa ujumla kusoma alama za nyakati kwa kujiongeza kufanya kazi.

 

Akipiga stori mbili tatu na Showbiz Xtra, Chopa alisema hadi sasa serikali ya awamu ya tano, chini ya Rais Dk John Magufuli imeshaonesha dira ya Tanzania Mpya hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kufuata kasi ya rais.

 

“Hizi sio zile enzi za kuishi kwa kupiga mizinga. Ni wakati wa kila mtu katika eneo lake kuhakikisha anafanya kazi sana, anaongeza ubunifu ili kuendana na kasi ya rais wetu,” alisema Chopa.

MWANDISHI WETU

Comments are closed.