The House of Favourite Newspapers

PAPII: MTOTO WANGU ANANIPA USHUJAA

MWANAMUZIKI mahiri wa Dansi Bongo, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ anaona fahari na ushujaa kila anapomuangalia mtoto wake, Asha ambaye alimuacha akiwa mdogo wakati akitumikia kifungo.

 

Akizungumza na Amani, Papii alisema kuwa, alipokuwa gerezani takriban miaka 14, hakupata muda mzuri wa kukaa na mtoto wake huyo zaidi ya alivyokuwa akienda kumsalimia gerezani, lakini kwa sasa ameona afanye kila analoweza mwanaye aweze kufaidi angalau matunda na furaha aliyoikosa kwa muda mrefu kutoka kwake.

 

“Unajua sijakaa na mtoto wangu kwa kipindi kirefu sana na hivi sasa ndiyo anatakiwa afaidi matunda kutoka kwa baba yake hivyo ni lazima nifanye kazi kwa jasho jingi ili ayafaidi matunda yangu,” alisema Papii.

 

Hata hivyo, Papii amewaomba mashabiki wake wajitokeze kwa wingi kwenye shoo yao inayotarajiwa kufanyika Machi 10, mwaka huu katika Ukumbi wa King Solomon, Namanga jijini Dar.

IMELDA MTEMA

Comments are closed.