The House of Favourite Newspapers

China Yamfukuza kazi Waziri wake wa Ulinzi Li Shangfu, Kufanya mkutano wa usalama

0
Li Shangfu

China imemfukuza kazi Waziri wake wa Ulinzi Li Shangfu miezi miwili tangu kutoweka kwake kwenye maisha ya umma.

Hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuhusu hatua hii, na vilevile mrithi wa nafasi hiyo hajatajwa.

Kufukuzwa kazi kwa Shangfu kumeiacha China bila Waziri wa Ulinzi wakati ambapo nchi hiyo ikijiandaa na mkutano mkubwa wa maafisa wa usalama unaofanyika wiki hii huko Beijing.

Hivi karibuni China imekuwa ikiwafukuza kazi viongozi kadhaa wa juu akiwemo Qin Gang ambaye alifukuzwa kazi kama Waziri wa Mambo ya Nje mwezi Julai.

Bw.Qin na Li pia wamefukuzwa katika nafasi zao kwenye Baraza Kuu la Taifa.

Wabunge wakuu wa China pamoja na kamati ya National People’s Congress (NPC) ambacho ndicho chombo cha juu zaidi cha Mamlaka katika Serikali ya China, wameafiki uamuzi huo.

PASUA KICHWA! UTEUZI wa MAKONDA, WAGAWA VIGOGO/ CCM WAHUJUMIANA/ KESI AKINA MDEE MBELE TENA

Leave A Reply