The House of Favourite Newspapers

CHINA YASHEREKEA MIAKA 70 TANGU KUANZISHWA KWA JAMHURI YAO NCHINI TANZANIA

Balozi wa China nchini, Wang Ke akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza jambo kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea katika hafla hiyo.
Kutoka kushoto ni makamu wa chama cha mapinduzi (CCM), Philip Mangula, Waziri mkuu mstaafu, Mizengo  Kayanza Peter Pinda na  Waziri wa katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga.
VIONGOZI mbalimbali walihudhuria hafla fupi ya raia wa China kupitia ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kusherehekea miaka 70 tangu kuanzishwa kwa jamhuri wa watu wa China ambapo waliishukuru Tanzania kwa kuendelea kuwa na mahusiano bora ya kidiplomasia kwa miaka 55 sasa.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi amewapongeza raia wa china kwa kudumisha jamhuri hiyo ambapo imewanufaisha wananchi wengi kwa takribani miaka  70  wamefanya mapinduzi makubwa kwa uchumi na kuwa kati ya nchi tano zenye watu wengi zaidi na moja kati ya nchi ambazo zina uchumi mkubwa na imara duniani.
Prof. Kabudi amesema kuwa China imekuwa nchi yenye gunduzi nyingi ambazo pia husaidia mataifa mengine hasa katika sekta za viwanda, biashara na teknolojia na wamekuwa wakiishawishi Tanzania katika kuyafikia malengo yao ya maendeleo ya mwaka 2025.
Vilevile amesema kuwa wanaposherekea miaka 70 ya tangu kuanzishwa kwa jamhuri hiyo pia wanasherekea miaka 55 ya mahusiano bora ya kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili, amesema kuwa nchi hizo zimekuwa zikishirikiana kwa ukaribu zaidi na mahusiano hayo yamekuwa mahusiano ya kindugu na ametoa pongezi kwa marais wa nchi hizo mbili wameendelea kudumisha mahusiano bora ya kidiplomasia.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini, Wang Ke amesema kuwa kipindi chote cha miaka 70 nchi hiyo imepitia vipindi kadhaa katika kulitoa taifa kutoka hali ya chini hadi kujenga uchumi imara ambapo kwa sasa China ni nchi ya pili duniani kiuchumi pamoja uzalishaji kwa ujumla.
Amesema kuwa hali za maisha kwa wananchi zimeendelea kuimarika na hiyo ni pamoja na kuendeleza amani, na sio vita pamoja na  kuweka mbele zaidi shughuli za maendeleo ili kuweza kuondokana na umaskini.
Wang Ke amesema kuwa mwaka huu pia wanasherekea miaka 55 ya mahusiano bora ya kiplomasia baina ya Tanzania na China na kueleza kuwa nchi hizo zimekuwa zikishirikiana kwa karibu katika kuhakikisha maendeleo na huduma muhimu zinawafikia wananchi, na amehaidi kuendeleza mahusiano hayo yataendelea kudumishwa.
Pia Wang Ke amempongeza Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini China na Waziri Mkuu mstaafu  Dkt. Salim Ahmed Salim kwa kupewa medali ya heshima ya urafiki wa kidiplomasia iliyotolewa na Rais wa China Xi Jinping mapema wiki hii, Wang amesema kuwa balozi Salim ni rafiki mzuri kwao na alikuwa na miaka 27 pekee alipoanza kuiwakilisha Tanzania nchini humo.
Amesema wataendelea kushirikiana na Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika ili kuweza kuyafikia malengo ya maendeleo ya mwaka 2063.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Tulia Ackson, Waziri wa katiba Balozi Augustine Mahiga, Waziri mkuu mstaafu, Mizengo  Kayanza Peter Pinda, makamu wa chama cha mapinduzi (CCM), Philip Mangula, majeshi ya ulinzi na viongozi mbalimbali wastaafu.

Comments are closed.