The House of Favourite Newspapers

Chombo cha Nasa Kuchukua Sampuli Sayari ya Mars

0

WANASAYANSI wanasema ni fursa yao bora ya kubaini iwapo sayari Mars iliwahi kuhifadhi maisha viumbe ni kufanyia uchunguzi sehemu ya juu ya ardhi na miamba katika maabara za kisasa.

Kifaa kidogo chenye ukubwa wa kidole cha mkono, kitafungwa kwenye mrija mdogo kwa ajili ya kurejeshwa hatimaye duniani. Chombo hicho kinachofahamika kama Perseverance kilitua kwenye sayari nyekundu mwezi Februali, kwenye kreta yenye upana wa kilomita 45 (maili 30 ) iitwayo Jezero.

Huu ni mkusanyiko wa rangi ya miamba chakavu ambayo wana sayansi wanaamini kuwa inawakilisha sakafu ya kreta za sayari ya Mars zinazofahamika kama Jezero. Picha za setilaiti zinaonesha eneo la chini la mahala ambapo paliwahi kuwa ziwa wakati mmoja, lililojazwa kwa mto wa aina ya delta.

 

Kutokana na hili, eneo hili linachukuliwa kama eneo ambalo huenda liliwahifadhi viumbe wadogo wa kale (kama walikuwepo katika sayari hiyo). Roboti ya Nasa imejiendesha Kilomita 1 (sawa na futi 3,000) Kusini kutoka mahala ambapo ilitua miezi mitano iliyopita. Nasa inafurahia jinsi chombo cha Perseverance kinavyofanya kazi.

Leave A Reply