Chongolo Azitaka Mamlaka za Usimamizi Miradi ya Serikali Morogoro Kuwa Makini
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amezitaka mamlaka za usimamizi za serikali Mkoa wa Morogoro kusimamia kwa ukamilifu miradi ya miundombinu ya serikali katika mkoa huo kwa sababu serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi za miradi ambazo zinatokana kodi za wananchi masikini.
Chongolo ameyasema hayo akiwa katika ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM Wilaya ya Gairo ambapo amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi na Mbunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby kuwa madaraja matatu katika Kijiji cha Nguyami yamebomoka kwa vipindi vitatu kutokana na kujengwa chini ya kiwango.