The House of Favourite Newspapers

CHRIS BROWN ATAJWA KUWA KWENYE MAHUSIANO NA INDYA MARIE

MWANAMUZIKI wa marekani anayebamba na ngoma ya ‘Wobble Up’,  Chris Brown,  anatajwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanamitindo Indya Marie . Wawili hao walianza kuwa karibu mwaka 2015 baada ya Chris Brown kuachana na  mpenzi wake Karrueche Tran. Hivi karibuni wameonekana wakiwa  pamoja katika  kuandaa video mpya  ya ‘Type a Way’ ya Eric Bellinger Ft Chris Brown.
Chris  na Indya  walionekana wakishikana mikono  katika pozi za mahaba na kuelekea kwenye After Party ya Chris Brown. Mitandao ina maswali mengi kama Indya ataweza kuziba pengo la Rihanna, Karrueche na kuwa mama kwa mtoto wa Chris Brown, Royalty.

Comments are closed.