The House of Favourite Newspapers

CHRIS BROWN AWEKA WAZI TAREHE YA KUACHIA ALBUM YA INDIGO


MWANAMUZIKI wa Marekani Chris Brown kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameweka wazi Tarehe Rasmi ya kuachia Album yake mpya ya “INDIGO” ambayo imekuwa ikisubiliwa kwa hamu na mashabiki zake Tarehe 21 June ndio siku itakayotoka iyo Album.

 

Chris Brown ameweka picha mbili amabazo ni cover ya iyo Album ikionesha muonekano wa mbele pamoja na nyuma ikiwa na michoro tofauti ya Pyramid kwenye upande wa nyuma.


Album ya Indigo itakuwa  na jumla ya ngoma 30, Album hiyo inatajwa kujumuisha ngoma ambazo tayari zimeshaachiwa ikiwemo “Undecided,” ”Back to Love” , na itawashirikisha wasanii 15 Drake, Nicki Minaj, Lil Wayne, Juvenile, Joyner Lucas, G-Eazy, Tyga, Juicy J, Gunna, Tory Lanez, Justin Bieber, Lil Jon, Tank, H.E.R. na Sage The Gemini.

Comments are closed.