The House of Favourite Newspapers

CHRIS ZYLKA AMTAKA PARIS ARUDISHE PETE YA UCHUMBA

LICHA ya uchumba baina ya waigizaji na mastaa Wamarekani,  Chris Zylka na Paris Hilton, kuvunjika karibu mwaka mmoja sasa, bado aliyetegemewa kuwa biharusi (Paris) anayo pete ya uchumba ya thamani ya Dola mil. 2 (Sh. bil. 2.6).

Imefahamika kwamba Paris ndiye aliyevunja uchumba huo, na kwa sheria za California, kwa kuwa mwanamke ndiye aliyevunja uchumba, itabidi mwanamme arejeshewe pete yake.  Hivyo,  Chris anaitaka pete hiyo yenye uzito wa ‘carat’ 20 za almasi ambayo ilichukua miezi minne kuichonga.

Ajabu ni kwamba, pamoja na kwamba kitu hicho chenye thamani kingekuwa salama kwenye kidole cha Paris, pete hiyo ilipotea na baadaye kupatikana tangu Chris alipopendekeza uchumba huko Aspen, Colorado.

 

Comments are closed.