The House of Favourite Newspapers

Christian Bella Kufanya Balaa Tamasha la Full Moon Party, Leo

0

Mkali wa muziki wa dansi nchini, Christian Bella na Bendi yake ya Malaika leo anatarajiwa kuzindua tamasha la Full Moon Party katika Ufukwe wa Dynasty uliopo Ununio Jijini Dar na kupambwa na warembo wa Miss Utalii.

 

Akizungumza na mwanahabari wetu mratibu wa tamasha hilo, Manase Mwakale amesema maandalizi yote ya tamasha hilo yameshakamilika ambapo pamoja na Bella kutakuwa na wasanii wengine watakaoibuka kama sapraiz kwenye tamasha hilo.

Mratibu wa onesho hilo, Manase Mwakale (katikati) akiwa na baadhi ya warembo watakaonogesha tamasha hilo.

Manase ameendelea kusema kuwa tamasha hilo litaanza jioni na kuendelea mpaka majogoo ambapo usalama wa watu na mali zao utakuwepo.

 

Akizungumzia lengo la tamasha hilo mratibu huyo amesema tamasha kama hilo yaani Full Moon Party lina maana ya mwezi mpevu au kipindi ambapo mwezi kuwa na mwangaza mkali hufanyika sana nchi zilizoendelea haswa barani la Ulaya, Amerika, Asia na kwingineko lengo likiwa ni walengwa kupata nafasi ya kupumzisha akili baada ya pilika za kutafuta maisha.

Mmoja wa mamisi akiwa kwenye chumba cha kufanyia masaji ufukweni hapo.

“Hivyo Christian Bella ndiye atakayetuzindulia tamasha hili leo hapa Dynasty Ununio baada ya hapo kutakuwa na muendelezo wake ambao tutakuwa tukiwajulisha wadau kila tutakapoandaa tena na kuwaambia wasanii tofauti tutakaowaalika huku tukichukua na maoni yao juu ya wasanii wanaowahitaji”. Alisema mratibu huyo.

 

Manase alimalizia kwa kusema kwenye kiwanja hicho kipya kuna huduma mbalimbali ikiwemo sehemu ya malazi, kufanyiwa masaji na mamisi na burudani zingine. Alimaza kusema mratibu huyo.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL 

Leave A Reply