The House of Favourite Newspapers

Chunga Sana Ndoa Haitaji Kuzoeana

0

NA ERICK EVARIST | RISASI JUMAMOSI | LOVE STORY

VIPO vitu vingi ambavyo kadiri unavyovifanya sana, ukavizoea, vinaleta tija lakini asikwambie mtu ndoa haihitaji mazoea. Ndoa inatakiwa kuwa mpya kila siku. Kama ni kujifunza, kwenye ndoa unapaswa kujifunza kila wakati. Kila siku umuone mwenzi wako kama mpya vile.

Kama ndiyo kwanza mmeonana. Chukulia kama vile ndiyo umemuona kwa mara ya kwanza, unavyokuwa na kile ‘kiraruraru’ cha kumhitaji.

Nasema hivyo marafi ki zangu kwa sababu mimi na wewe ni mashahidi katika hili. Tunashuhudia namna ambavyo matatizo yanavyotokea. Watu wanagombana, watu wanashitakiana kila kukicha, watu wanaachana.

Ukichunguza kwa makini, chanzo kikubwa cha watu kufi kia hatua hiyo ni mazoea. Wameishi miaka mingi, wamezaa, wamezoeana kupita kiasi. Mke hana habari tena na mume. Mume naye ndiyo usiseme, hana muda na mke.

Wanachukuliana poapoa tu. Kinachotokea, kama zamani walikuwa wana tabia ya kujaliana kila wakati, inafi ka wakati wanaacha. Walikuwa wanapigiana simu kila wakati, inafi ka wakati hawapigiani hata siku mbili tatu. Wanapigiana pale panapokuwa na jambo la msingi tu. Mtoto anaumwa, ada inahitajika haraka na mambo mengine yanayofanana na hayo. Zile za kuulizana ‘baby unakula nini leo’, ‘mpenzi nikuletee zawadi gani’ zinakoma kabisa.

Mke anakuwa bize na marafi ki zake. Mume naye anakuwa bize na marafi ki zake. Ndoa itawakutanisha jioni au usiku. Usiku wenyewe kila mtu akifi ka anakuwa na hamsini zake. Wanalala kama vile mtu na kaka dada yake. Hiyo yote yanaletwa na mazoea.

Mke anamzoea mume wake hadi inafi ka wakati anapoteza hamu naye. Anamuona wa kawaida. Awepo sawa, asiwepo hewala. Vivyo hivyo mume. Naye anamuona mke kama vile mtoto wa ba mkubwa. Nyumbani mke hana muda na mume.

Akirudi mambo yote anamuachia dada wa kazi. Aandae maji ya kuoga, chakula na hata usafi wa chumbani kwao.

NI RAHISI KUTAMANI MTU MWINGINE

Kadiri mazoea yanavyozidi kushika hatamu, ni rahisi sana mke kumtamani kijana sharobaro kutokana na namna ambavyo anajua kujali hata kwa kuuliza vipi umeamkaje?

Vipi unaendeleaje?

Mtoto hajakusumbua sana leo usiku?

Acha nikusaidie kubeba hii ndoo ya maji na mambo mengine yanayofanana na hayo. Hii haina tofauti na yule fundi ambaye anamwita na kutokea kwa wakati pale gari lake linapokuwa limeharibika barabarani. Gari kanunuliwa na mumewe lakini fundi anakuwa mwepesi sana kufi ka au kutoa msaada eneo la tukio kuliko mume.

Fundi anajali adha anayoipata mke wa mtu barabarani kuliko mwenye mke, ana bidii ile mbaya. Mwenye mke akipigiwa simu na mkewe kuambiwa kwamba gari imeharibika, anachukulia poa. Majibu ni yale ya ‘sasa mimi nifanyeje?

Si umuite fundi?’

Hayo ndiyo mazoea yenyewe!

 

Mume anasahau kwamba mke anafahamu kwamba yeye si fundi lakini amempa taarifa kama mtu wake wa karibu.

Mtu ambaye anaamini atampa jibu lenye msaada. La kumpa matumaini, la kumtia moyo lakini matokeo yake anaambulia maneno ya shombo. Mazoea yanasukuma hata suala la faragha liwe la kawaida tu. Liwepo lisiwepo yote heri.

Wanaishi pamoja hata miezi miwili, hakuna anayemgusa mwenzake. Matokeo yake, atazidiwa na matamanio na akapata mtu wa kumtamani, anampa nafasi. Akimpata mtu anayejua kujali, anayejua ‘vurugu za mapenzi’ anashawishika. Anajikuta huko sababu tu ya mazoea mliyoyaweka. Usaliti unakua na hata kuhatarisha ndoa, achilia mbali uwezekano wa kupata magonjwa.

ACHA MAZOEA

Kama vile mlivyoonana, mnapaswa kuishi hivyo miaka yote. Chukulia kama ni jukumu. Usiufanye uhusiano wako uchache. Kila siku uamshe kwa staili tofauti. Kama ulikuwa una tabia ya kumtoa ‘out’, zidisha kasi.

Kama ulikuwa unamthamini kwa shida na raha basi hayo ndiyo yawe maisha yako. Mpende, mdekeze ikibidi maana huyo ndiye wako. Hakuna mwingine. Dekezaneni kila inapobidi maana hakuna namna. Kila mmoja awe na hamu na mwenzake kila wakati.

Usichukulie poa, thamani ya mke au mume inapaswa kuwa vilevile kila siku. Kila mmoja aguswe na maumivu ya mwenzake. Mkianguka kwenye shida muwe pamoja na mkiwa kwenye raha basi mfurahi pamoja. Heshimuni ndoa, iwekeni mbele na muipe thamani kila uchwao! Mkiishi kwa staili hiyo, maisha mtayaona matamu na hakuna kitakachowayumbisha!

Leave A Reply