The House of Favourite Newspapers

Cloud 112: Nafurahia maisha ya ndoa

0
Cloud 12 akiwa na familia yake.

 

MAMBO vipi shabiki namba moja wa Mpaka Home? Natumai upo poa sana. Kama ilivyo ada ya safu hii ni kutinga nyumbani kwa mastaa wa Bongo na kuyadadavua maisha yao halisi ya kila siku nje ya fani zao zilizowatambulisha kwenye jamii.

Wiki hii tunaye muigizaji mkali ambaye alipotea takriban miaka mitatu akiwa ughaibuni katika nchi ya Sweden, Issa Musa ‘Cloud 12’.

Lakini sasa amerejea Bongo akiambatana na mkewe anayejulikana kwa jina la Amina na watoto wao wawili. Maisha yao ya muda wameyafanya Tabata-Baracuda jijini Dar. Safu hii imezungumza na Cloud mambo mengi, ungana nami hapa chini;

 

Akiwa na mkewe

 

Mpaka Home: Mambo vipi Cloud, habari za siku nyingi?

Cloud: Salama, Bongo mnasemaje?

Mpaka Home: Niko hapa kwa ajili ya kujua maisha yako halisi nje ya kazi yako ya uigizaji, japokuwa najua maisha yako kwa sasa, kwa asilimia kubwa yapo nchini Sweden. Lakini kwa vile hapa ni nyumbani, pia wapenzi wako wangependa kujua ratiba yako ya siku nzima?

 

 

Cloud: Kwanza kabisa mimi napenda sana kumuabudu Mungu kwa kila jambo hivyo kabla ya kufanya chochote, huwa naanza kusali kwanza na vitu vingine vinafuata.

Mpaka Home: Nakuona mpaka usoni imejitokeza sijda.

Cloud: Ni kweli kabisa maana mimi ninaona bila Mungu hakuna kitu kabisa.

Mpaka Home: Unapenda kufanya nini unapokuwa umepumzika nyumbani?

Cloud: Napenda sana kumsaidia mke wangu kazi za nyumbani kama kupika na vitu mbalimbali maana huko kwa wenzetu, wanaume wanasaidia wake zao kila kitu.

Mpaka Home: Ni kitu gani ambacho kinakupa furaha?

Cloud: Kuona mimi na mke wangu kuna maelewano, hicho ndicho kitu kikubwa zaidi na ninakifurahia. Mpaka Home: Nimekuona jikoni ukiwa karibu na mkeo ukimsaidia kazi mbalimbali tofauti na mastaa wengine, unalizungumziaje hilo maana watu hawachelewi kusema wewe ni mume bwege?

Cloud: Watu watakaosema hivyo ni malimbukeni kwa sababu Sweden ni kitu cha kawaida kwani ni lazima kumsaidia mke wako maana hata kwenye vitabu vya dini ipo hiyo.

Mpaka Home: Kitu gani ambacho hukipendi na kinakuchukiza unapokuwa nyumbani?

Cloud: Sipendi mtu kunitafsiri ndivyo sivyo, nachukia sana mtu kukukopa pesa zako halafu wakati wa kulipa inakuwa shida.

 

 

Mpaka Home: Ni chakula gani unapenda kula na pia inapofika wakati wa jioni unafanya nini?

Cloud: Ninapenda sana kula vyakula vya kawaida kama samaki, ugali na hata wali kwa sababu kule Sweden mara nyingi vinapatikana kama huku tu. Wakati wa jioni mazoezi yamekuwa ni sehemu kubwa pia kwangu au kutembea.

Mpaka Home: Vipi maisha yako ya ndoa hii mpya maana mwanzo najua ulioa pia?

Cloud: Nayafurahi sana maisha ya ndoa. Ninamshukuru Mungu kwa kunipatia mke mwema na mcheshi kwa kila mtu.

Mpaka Home: Mna mpango wa kurudi kuishi nyumbani Bongo moja kwa moja?

Cloud: Hapana, kwa vile hapa ni nyumbani tutakuwa tunakuja na kurudi Sweden.

Mpaka Home: Okey, ninakushukuru sana kwa ushirikiano wako.

Cloud: Karibu sana.

Leave A Reply