The House of Favourite Newspapers
gunners X

Corona: Masanja Mbele ya DC Katambi “Hata Kanisani Nafanya” – Video

0

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amemsamehe mchekeshaji Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ baada ya kuitikia wito wake alioutoa wa jana Aprili 3, 2020 wa kufika ofisini kwake au Polisi kwa madai ya kutumia utani kuwahoji wananchi kuhusu uelewa wao juu ya Ugonjwa wa Corona (Covid – 19).

Akizungumza na Wandishi wa habari, Masanja amesema lengo la kipindi lilikuwa kuelimisha na siyo kuleta mzaha, na ameomba radhi kwa hilo.

Pia, amemuahidi DC Katambi kuwa atatumia kipawa chake kuhamasisha watanzania kutumia vitakasa mikono na kufuata masharti yote ambayo yanatolewa na viongozi kuhusu #CoronaVirus.

DC Katambi amesema hana tatizo binafsi na Masanja wala kituo cha DW ambacho muigizaji huyo anafanyia kazi bali walimuita kwa ajili ya kuwekana sawa.

Alichojibu Masanja Mbele ya DC Katambi, Sakata la Kutania CORONA “Hata Kanisani Nafanya”

Leave A Reply