The House of Favourite Newspapers

COSOTA, RUGE MUTAHABA FOUNDATION KUTOA ELIMU YA HAKIMILIKI KWA VIJANA MILIONI 1

0
Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) imesaini makubaliano ya ushirikiano (MoU) na taasisi ya Ruge Mutahaba Foundation kufanya Kampeni ya kutoa Elimu ya Hakimiliki.
Akizungumza kuhusu Kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa COSOTA Bi. Doreen Sinare amesema itatambulika kama “HAKIMILIKI YAKO HAILIKI, KAMATA FURSA TWENZETU”
Kampeni hiyo imezinduliwa  rasmi Mei 09, 2024 Jijini Dar es Salaam katika siku ya Maadhimisho ya Miliki Ubunifu Duniani.
Kwa mujibu wa Sinare  Kampeni hiyo imelenga kutoa elimu kwa wabunifu hasa vijana wanaofanya kazi za Sanaa, uandishi na  ubunifu unaohusiana na hakimiliki unaolindwa na Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 1999 pamoja na marekebisho yake kama Ubunifu wa mifumo, muziki, filamu, sanaa za maomesho, uandishi, matangazo, picha na michoro.
Makubaliano ya pande hizo mbili yatadumu kwa  kipindi cha miaka mitatu na yamelenga kufikia vijana 1,000,000 na kuongeza usajili wa kazi zinazolindwa na hakimiliki.
Kupitia Mkakati wa Maboresho ya Mazingira ya Biashara (MKUMBI)  unaosimamiwa na Ofisi ya Rais, Mipango na Uwezeshaji chini ya  ufadhili wa Umoja wa Ulaya (European EU) COSOTA itaendelea kutoa elimu ya hakimiliki.
Leave A Reply