The House of Favourite Newspapers

Country Boy: Bila Bifu Hakuna Muziki

Ibrahim Mandingo ‘Country Boy’

RAPA Ibrahim Mandingo anayefahamika zaidi kwa jina la ‘Country Boy’, amefunguka kwamba bila wanamuziki kuwa na bifu hakuna msisimko kwenye muziki, kwani anaamini ushindani wowote unatokana na tofauti wanazokuwa nazo watu wawili wanaofanya kitu kinachofanana.

 

Akichonga na Star Showbiz, Country Boy alisema kuwa, msisimko kwenye muziki unapungua kwa sababu wanamuziki wengi kwa sasa wanaogopa masuala ya bifu bila kufahamu wanalikosesha soko msisimko ambao ungekuwepo kama kunapotokea tofauti.

 

“Unajua muziki ni mashabiki, sasa kunapokuwa na wanamuziki wawili wana tofauti hata mashabiki wao pia wanakuwa wanashindana na kutamba kuonesha kwamba mwanamuziki wao ni mkali kuliko yule mwingine.” Alimaliza.

STORI: BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.