The House of Favourite Newspapers

Umuhimu wa Samaki kwa Watoto Wachanga

SAMAKI ni kitoweo ambacho kinatajwa kuwa na mafuta yenye kiambata aina ya Omega 3 yanayomfanya binadamu kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri, kutunza kumbukumbu na kuishi kwa muda mrefu.

 

Vyakula vyote vinavyozalishwa majini huwa na kiambata aina ya Omega 3 yenye mafuta yatokanayo na samaki yanayotakiwa kwa mwili wa binadamu, yana mbegu maalumu zinazomsaidia binadamu katika ukuaji ambazo pia ni maalum kwa faida ya mfumo wa ubongo na neva.

 

Samaki wana kiambata aina ya Omega 3 ambayo husaidia katika ukuaji wa binadamu na kujenga ubongo wake vizuri, ndiyo maana watu wanaoishi katika maeneo yaliyozungukwa na maji mengi ‘bahari, mito au maziwa’ ni watu wenye akili nyingi na watambuzi hata kama hajaenda shule na akienda shule hufanya vyema sana darasani.

Kinamama wajawazito kwa upande wao wamekuwa wakipewa ushauri kutumia kitoweo hicho, wanapaswa kula samaki kwa wingi ili kukuza ubongo wa mtoto tumboni, pia ni lazima wale nyama nyekundu ili kuongeza damu kwa uharaka mwilini ila tunawashauri isizidi nusu kilo kwa siku saba.

 

Omega 3 humsaidia mtoto kukuza ubongo, kutengeneza retina kwenye mboni ya macho na kutengeneza mfumo wa neva. Pia, humsaidia mama kuzuia matatizo kama kifafa cha mimba na sonono baada ya kujifungua.

 

Njia kuu ya mtoto kupata Omega 3 ni kutokana na vyakula anavyokula mama yake, hivyo ale samaki kwa wingi.Kama mama atashindwa kupata vyakula vya kutosha vyenye Omega 3, basi mtoto atachukua ile iliyoko mwilini mwa mama ambayo mara nyingi iko kwenye ubongo wa mama.

 

Samaki wana umuhimu katika afya ya mama na mtoto na iwapo mama hatapata Omega 3 ya kutosha anaongeza hatari ya kupata mtoto mwenye uzito mdogo, uchungu wa mapema, mtoto kuzaliwa kabla ya muda, au kulazimika kuzaa kwa upasuaji.  Watoto ambao wamepata Omega 3 ya kutosha wameonyesha kuwa na umakini mkubwa na upeo mzuri kuliko watoto wengine wasiopata Omega 3.

 

Pia, hukua kwa haraka zaidi kuliko yule ambaye hakupata kiambata hicho na huwa mtunzaji mzuri wa kumbukumbu. Kwa watu wazima hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti na saratani nyinginezo.

 

 

Omega 3 inayopatikana kwa kula samaki inahitajika kwa kila binadamu ili kuendelea kuutunza ubongo na kujiepusha na magonjwa yanayotokana na kukosa madini haya. Ni vizuri kupata Omega 3 ya kutosha kupitia mlo wa kila siku.

 

Wakati wa ujauzito mwanamke anashauriwa kupata angalau gramu 250 kila siku na katika kipindi cha mwisho (miezi mitatu ya mwisho) kwa sababu katika kipindi hiki mtoto hutumia asilimia 70 ya Omega 3 kujenga ubongo wake na mfumo wake wa neva. Vyanzo vinavyoleta madini hayo vinapatikana katika samaki na mafuta ya samaki hasa samaki wenye mafuta mengi kama vibua, sato, salmon, sangara, dagaa na jodari.

Lakini kuna samaki wengine wana sumu, ni aina gani hao? Fuatilia Jumanne ijayo.

Comments are closed.