The House of Favourite Newspapers

Cristiano Ronaldo aweka rekodi nyingine kubwa duniani

Mshambuliaji wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo jana usiku ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tano wa muda wote duniani kufikisha magoli 700.

Goli la penati la Cristiano Ronaldo aliloifungia Ureno dakika ya 72 kwa penati katika mchezo wa kuwania kufuzu Euro 2020, linamfanya Ronaldo atimize jumla ya magoli 700 katika maisha yake ya soka (Sporting 5, Man U 118, Real Madrid 450, Juventus 32 na Ureno 95)

Comments are closed.