The House of Favourite Newspapers

Curry Aibuka Shujaa Stamford Bridge

0
Stephen Curry

STAA wa mpira wa kikapu Stephen Curry, juzi alionyesha uwezo wake kwenye mchezo wa soka baada ya kuwa mgeni kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Staa huyo alikuwa mwalikwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu England kati ya Chelsea dhidi ya Arsenal na kupewa nafasi ya kuingia uwanjani ambapo alionyesha uwezo mkubwa wa kupiga mkwaju wa penalti.

 

Staa huyo wa Golden State Warriors, inayoshiriki Ligi Kuu ya Kikapu Marekani, (NBA), alionyesha kiwango cha hali ya juu sana kwenye msimu wa ligi hiyo uliopita.

 

Curry, amewahi kutwaa tuzo ya NBA MVP mara mbili na kutwaa ubingwa wa ligi hiyo mara mbili, jambo linalomweka kwenye hadhi ya juu sana kwenye mchezo huo.

 

Curry ambaye anaaminika kuwa ni shabiki wa Chelsea, aliangalia mchezo huo kwa dakika tisini na baada ya kumalizika alishuka uwanjani ambapo alichukua mpira na kipa akakaa langoni ambapo alipiga penalti matata sana na kufunga huku mashabiki wachache wakimshangilia.

 

Curry, ambaye wastani wake kwenye NBA ni pointi 25.3 kwa mechi, asisti 6.6 na rebaundi 4.5 kwa kipindi chote cha mapumziko alikuwa akifurahia soka ambapo alionekana kwenye viwanja mbalimbali ukiwemo mchezo wa kwanza wa Neymar kwenye kikosi cha PSG.

Leave A Reply