The House of Favourite Newspapers

Curry; Hili Ndiyo Bata la Ushindi Sasa!

0

BATA BATANI! Mcheza kikapu wa Timu ya Golden State Worriors ambao walichukua ubingwa wa NBA wiki iliyopita, Steph Curry ameamua kwenda kusherehekea ushindi huo ufukweni katika Visiwa vya Hawaii nchini Marekani huku akiwa na familia yake.

Watu waliokuwa hapo ufukweni, walifurahia kumuona huku wengine wakisema kwamba amekuwa mzuri katika kunywa bia na kuvuta sigara, kutupiana kopo za bia hizo huku watoto wake wakizidaka kitu kilichofananishwa kwamba akiwa uwanjani, mpira anamrushia Kevin Durant kufunga ila kwa hapo watoto wake wanahusika sana kwenye kudaka kopo hizo.

Ikumbukwe kuwa Golden State Worriors walichukua ubingwa wa NBA baada ya kuwafunga Cavaliers katika michezo minne badala ya saba ambayo walitakiwa kucheza.

 

 

 

 

 

Na: Nyemo Chilongani

Leave A Reply