The House of Favourite Newspapers

Daktari Matatani kwa Kuwapapasa, Kuwabusu Wagonjwa Wake Wakiwemo Wajawazito

0
Krishna Singh Daktari kutoka North Lanarkhire nchini Scotland, ambaye amekutwa hatia ya makosa 54 ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya Wanawake

DAKTARI mmoja kutoka North Lanarkhire nchini Scotland, Krishna Singh (72) amekutwa na hatia ya makosa 54 ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya Wanawake kwa zaidi ya miaka 35 iliyopita.

 

Singh anatuhumiwa kuwabusu, kuwapapasa na kuwafanyia uchunguzi usiofaa na kutoa maoni ya uzembe kwa wagonjwa 48 wakati alipokutana nao katika mazingira mbalimbali ya matibabu.

 

Wagonjwa hao ni pamoja na mwathiriwa wa ubakaji, wasichana na wanawake wajawazito, Singh amepatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono na vitendo vya aibu ambayo alivifanya kati ya Februari 1983 na Mei 2018.

 

Singh hakuthibitishwa kukosa katika mashtaka mengine tisa na amekutwa bila hatia kwa mashtaka mengine mawili, Jaji anayesimamia kesi hiyo Lord Armstrong amesema hukumu itatolewa mwezi ujao.

 

Leave A Reply