The House of Favourite Newspapers

Dance Club Yazindua Kampeni Simba Na Yanga Kuelea Robo Fainali Club Bingwa Afrika

0

Dar es Salaam, 21 Machi 2024: Baa ya Dance Club iliyopo Mwenge Mpakani jijini Dar es Salaam, imezindua kampeni maalum kwa ajili ya kutoa fursa kwa mashabiki wa timu za Simba na Yanga kutoa hamasa kwa timu zao wakati wa michezo ya robo fainali ya Club Bingwa Afrika na kueleka mpaka nusu fainali na fainali endapo zitafuzu.

Kampeni hiyo inayojulikana kama “Mpaka fainali inawezekana” Dance tuvushe! inalenga kutoa hamasa kwa wateja wa Dance Club ambao ni mashabiki wa Simba na Yanga kuhakikikisha wanahamasika katika kushangilia timu zao kufika fainali za Club Bingwa Afrika.

“Lengo letu ni kuwafanya wateja wa Dance Club ambao ni mashabiki wa michezo hususani wa timu za Simba na Yanga kuwa katika mazingira mazuri na pia kuhakikisha wanafuatilia mpira moja kwa moja (live) katika screen kubwa na za kutosha Ndani ya Dance Club,” anasema Jaffary Lucas ambaye ni Meneja burudani wa Club hiyo.

Kwa mujibu wa Jaffary wateja  wa Dance Club ambao ni mashabiki wa Simba na Yanga na wepenzi wa mchezo wa soka kwa ujumla wataweza kununua kadi ambazo ni Green na Red card za Dance club sport funs.

“Wateja wetu wataweza kutumia kadi hizo kuingia kuangali mpira na kushangilia timu zao bila kiingilio na kubugudhiwa lengo likiwa ni ⁠kuongeza uzalendo kwa timu zetu haşa katika kipindi Hiki cha uwakilishi wa Taifa pasipo kujali ushabiki,”. alisema.

Leave A Reply