The House of Favourite Newspapers

DAR LIVE KUMWAGA HEADPHONES ZA BEATS BY DRE, PASAKA

IKIWA ni sehemu ya shamrashamra za Sikukuu ya Pasaka (Aprili Mosi) Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar unatarajia kumwaga headphones kibao za Beats by Dre orijino kwa mashabiki watakaopakuwa ‘application’ mpya ya Global Publishers inayopatikana kwenye simu za mkononi.

Akizungumza na Mikito Nusu Nusu, mratibu wa shindano hilo, Edwin Lindege alisema kuwa hii ni fursa kwa watu wote watakaojitokeza ukumbini hapo na kinachotakiwa ni kujiunga na huduma hiyo na kuanza kutumia.

“Hata kwa wewe ambaye upo nyumbani hii ni fursa kwako ya kutumia application hii na ukawa mshindi ukaja kuchukua zawadi zako Dar Live. Unachotakiwa kufanya ili uweze kujishindia headphones hizi ambazo zipo nyingi sana ni kuhakikisha kwanza uwe unatumia simu ya mkononi yaani hizi za iOS (mfano iPhone) au hizi za Adroid (Sumsung, Tecno, iTel, Huawei, Sony na nyingine) kisha unaingia katika stores.

 

“Mfano kama wewe unatumia hizi za iOS yaani iPhone unatakiwa uingie sehemu ya App Store na kuitafuta application yetu ya Global Publishers kisha unaipakuwa na kuinstall na kuanza kutumia, lakini pia kama unatumia Adroid yaani hizi simu nyingine (siyo iPhone) unatakiwa kuingia Play Store na kuitafuta Global Publishers na kuipakuwa bila kusahau kuinstall na kuanza kuitumia. Ukifanikiwa kufanya hayo au kuifungulia ukiwa Dar Live unaweza kuwa sehemu ya washindi watakao jishindia headphones za Beats by Dre orijino kabisa zenye muziki mnene,” alimaliza Lindege.

Comments are closed.