The House of Favourite Newspapers

Dar: Watu 7 Wanaodhaniwa Kuwa Majambazi Wauawa

0

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limewauwa kwa kuwapiga risasi watu saba wanaoshukiwa ni majambazo katika eneo la Mwenge, Cocacola. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi, Lazaro Mambosasa, watu hao walikuwa wakitaka kufanya uhalifu kwenye ghala la GS Limited.

 

Watu hao wameuawa Mei 25, 2020 saa 6 usiku baada ya kurushiana risasi na Polisi. Polisi wamewakuta watu hao na mitungi ya gesi ya kuvunjia milango.

 

Taarifa ya kamanda mambosasa

Kuuawa kwa majambazi saba na kupatikana na Silaha moja bastol yemye risasi tatu.

Majambazi hao wameuawa 25 Mei 2020 majira ya saa sita usiku Maeneo ya Mwenge Cocacola, Majambazi 7 wakiwa kwenye Noah wakielekea kufanya uharifu kwenye ghala la GS Limited. Askari walipata taarifa kutoka kwa msiri. Walilifuatilia gari hilo kulingana na taarifa. Majambazi baada ya kuona wanafuatiliwa na wapelelezi wa kanda waliongeza mwendo. Gari la Polisi iliongeza mwendo pia.

Walikuwa wamejihami na wakaanza kufyatua risasi. Polisi wakajibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi wote saba. Wakakamatwa na kukutwa na mitungi miwili ya gesi ya kuvunjia Milango. Walipofikishwa Hospitali, Daktari akasema wamekata roho. Afande Mambosasa amewataka watanzania kila mmoja kufuata sheria ya nchi.

Hali ya Usalama

“Hali ya jiji la Dar ipo vizuri, na watu wapo huru kutembea popote hadi kwenye fukwe. Nawapongeza wananchi wanaoishi kwa kufuata sheria. Nawashukuru wote wanaotoa habari za Uhalifu. Hivi juzi pale Tegeta kuna Mama alipigwa risasi na hawa wahuni,” amesema mambosasa.

 

Kuhusu Mchekeshaji Idris Sultani, Kamanda Mambosasa amesema hayupo Kanda maalumu ya Dar es Salaam, hivyo aulizwe DCI kwa afande Misime ndiye anaweza kuliongelea.

Leave A Reply