The House of Favourite Newspapers

Daraja la Ubungo lageuzwa chimbo la wapiga debe, machokoraa, wamachinga!

Daraja la Ubungo
Wapiga debe wakiwa wamelala katika uvungu wa daraja hilo.

 

Daraja la Ubungo  lililo nje ya stendi kubwa ya mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi lililopo Ubungo jijini Dar, mbali na kutoa huduma ya kuvusha watu kutoka upande mmoja kwenda mwingine, baadhi ya wafanyabiashara wadogowadogo wa eneo hilo, watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na wapiga debe wamegeuza uvungu wa kivuko hicho kama sehemu ya kulala wakati wa mchana.

Daraja la Ubungo

Mtandao huu leo ulipata fursa ya kupita maeneo hayo na kukuta vijana wengi wakiwa wamechapa usingizi na ikaelezwa kuwa, wengi wao ni wale ambao usiku wanakesha.

Daraja la Ubungo

“Unaowaona hapo wamelala, kuna mateja, wamachinga, wapiga debe na watoto wanaoishi mazingira magumu,” alisema mmoja wa vijana aliyeongea na mtandao huu.

 

PICHA, HABARI: AMOS NYANDUKU| GPL

Comments are closed.