The House of Favourite Newspapers

Daraja Refu la Kioo Kuliko Yote Duniani

0
Daraja la vioo china.

 

HEBU vuta picha, unatembea kwenye daraja, tena la vioo, ukitazama chini unaona bonde lenye urefu wa zaidi ya mita 300, sawa na viwanja vitatu vya mpira vilivyounganishwa, ukitembea unahisi kama unataka kudondokea kwenye korongo hilo au unahisi vioo vinaweza kupasuka na ukadondoka, unaweza kupiga hata hatua moja?

Ni wachache wenye uthubutu huo lakini wengi, hasa wale wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo au hofu ya kupindukia, huishia kutambaa tu huku wakipiga kelele za kuomba msaada, hawana ujasiri wa kusimama na kutembea.

 

 

Hii si stori ya kutunga, ni kweli nchini China kuna daraja liitwalo Zhangjiajie Grand Canyon ambalo limejengwa kwa vioo tupu, hakuna mbao wala bati, yaani ukiachilia mbali vyuma vilivyolishikiza, sehemu iliyobakia ni vioo mwanzo mpaka mwisho na kuweka rekodi ya kuwa daraja refu la vioo kuliko yote duniani.

Daraja hilo ambalo linatajwa kuwa miongoni mwa maajabu ya ulimwengu, limejengwa na Kampuni ya Haim Dotan LTD kutoka nchini Israel na limeanza kutumika rasmi mwaka huu, 2017, likitajwa kuvutia zaidi ya watu 8,000 kila siku.

 

Daraja la vioo likibomolewa.

 

Daraja hili linaunganisha vilele viwili vya Milima ya Avatar (Filamu ya Avatar ilirekodiwa kwenye milima hii), likiwa na urefu wa mita 430 kutoka ng’ambo ya kwanza mpaka ya pili, likitajwa kugharimu zaidi ya dola 3.4 milioni, sawa na shilingi bilioni 7.6 za Kitanzania.

 

Vioo vilivyotumika, hasa sehemu ya kukanyagia, vimepangwa kwa matabaka matatu ya vioo vigumu, visivy-oweza kuvunjika hata vikipigwa na nyundo ngumu, vikiwa na uwezo wa kuhimili hata uzito wa gari lililojaza abiria bila kupasuka.

Daraja la juu.

 

Tangu kuzinduliwa kwake, limekuwa kivutio kikubwa kwa watalii, watu wanaofanya yoga au hata wanaoenda kufunga harusi, huku idadi ya watu waoga, wanaopatwa na mshtuko mkubwa, wengine presha zikipanda na kuwafanya wakimbizwe hospitali baada ya kufika kwenye daraja hilo, ikizidi kuongezeka.

Unaambiwa kabla ya kutaka kupita kwenye daraja hilo, lazima upimwe presha na uwezo wako wa kuhimili hofu, ukionekana woga umekuzidi, unazuiwa au unapewa watu wa kukusaidia kutembea!

Mr. Nice Afanyiwa Kitu Mbaya Gesti Uwanja wa Fisi Manzese!

Leave A Reply