The House of Favourite Newspapers

Davina Aanika Siri ya Wazo la Pafyumu Yake

Halima Yahaya ‘Davina’

STAA wa filamu za Kibongo, Halima Yahaya ‘Davina’ ameeleza alikopata wazo la kutoa pafyumu yenye jina lake na kufunguka kuwa alilipata alipokuwa Dudai alikoenda kwa ajili ya biashara ya nguo.

Akiongea na Risasi Jumamosi Davina alisema kuwa, akiwa Dubai watu wengi walimpigia simu na kumtaka awaletee pafyum na ndipo akabaini kupitia bidhaa hiyo anaweza ‘kupiga pesa’.“Kwa kweli namshukuru Mungu, mzigo haujatoka bado lakini watu wameitikia na kama utaingia nchini  nishapata oda nyingi, kumbe mtu akijaribu brand yake anao uwezo wa kufanikiwa.

“Mimi nimeona baada ya kujaribu kuitangaza, kila mtu anataka kununua pafyumu yenye jina langu,” alisema Davina ambaye mbali na pafyumu naye amejikita kwenye umama n’tilie ambapo anapika na kuuza chakula mwenyewe

Comments are closed.