The House of Favourite Newspapers

DAVINA AVUNJA KIAPO CHAKE MWENYEWE

Davina
Halima Yahya ‘Davina

MWIGIZAJI wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ ambaye mara kadhaa amenukuliwa akisema hana mpango wa kuolewa tena baada ya ndoa yake kuvunjika, hivi sasa amevunja kiapo hicho na kusema ataolewa mwanzoni mwa mwaka ujao.

 

Davina aliiambia Za Motomoto News kuwa ni kweli aliwahi kusema kwamba hana mpango wa kuingia tena kwenye ndoa, lakini kwa kuwa ni binadamu kwa sasa wakati umefika na tayari ana mchumba ambaye anatarajia kuingia naye kwenye ndoa mwakani.

 

“Ikiwa mimi ni binadamu niliyekamilika, siwezi kukaa hivi bila kuolewa tena milele, niliyoyasema mwanzo ni maneno tu, lakini kwa sasa tayari nina mchumba na Mungu akipenda nitaingia tena kwenye ndoa mwaka ujao,” alisema Davina.

STORI: Gladness Mallya, Dar

Comments are closed.