The House of Favourite Newspapers

DAVINA: KAMWE SIJIHUSISHI NA UNGA

 Halima Yahaya ‘Davina’

MUIGIZAJI mahiri wa Bongo Movies, Halima Yahaya ‘Davina’ amefungukia safari zake zake za Dubai akisema ni kwa ajili ya biashara halali na si biashara haramu ya madawa ya kulevya (unga).

Akizingumza na Amani kwa njia ya simu akiwa Dubai, Davina alisema kuwa, kila anapokuwa huko kibiashara na akaweka picha mtandaoni, watu humhisihisi kuwa anasafirisha unga, jambo ambalo kamwe hawezi kulifanya.

“Yaani mimi safari zangu ni kwa ajili ya biashara zangu tu na kuhusu kujihusisha na biashara haramu za madawa ya kulevya, mimi huwa nasikia kwenye redio na kwenye magazeti, sithubutu, maisha bado ninayataka,” alisema Davina bila kutaja biashara inayompeleka Dubai mara kwa mara.

Stori: Imelda Mtema.

Comments are closed.