The House of Favourite Newspapers

Davina: Magufuli ametunyoosha!

davinaIMELDA  MTEMA, Gazeti la Risasi Jumamosi, Toleo la Januari 21, 2017

MTOTO mzuri Bongo Movies, Halima Yahaya ‘Davina’, ameweka ‘plain’ kuwa uongozi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli si wa mchezomchezo kwani ili uweze kuishi, lazima utoke jasho kwelikweli tofauti na zamani ambapo mtu ulikuwa unaweza kupiga ujanjaujanja na maisha yakaenda.

Davina alifunguka hayo alipokuwa akitoa tathimini yake kuhusu hali ya kiuchumi alipokutana na mwanahabari wetu hivi karibuni ambapo alisema ili kuendana na kasi ya rais, inabidi wasanii wapambane kuwa na mianya mingine ya kibiashara kuliko kutegemea sanaa pekee.

“Kwa hali ya sasa hivi mtu akitegemea kazi ya sanaa peke yake itakuwa imekula kwake kwa sababu sanaa ya sasa hivi ili upate hela lazima ushurubike hasa. Hiki siyo kile kipindi cha kuishi mjini kwa kuungaunga tu halafu maisha yanaenda,” alisema Davina.

Comments are closed.