The House of Favourite Newspapers

DC Jokate Mwengelo Amwanika Mwanawe Amtambulisha Kwa jina la Totoo

0

Wiki mbili zilizopita, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwengelo aliachia picha ujauzito baada ya kujulikana kuwa ni mama kijacho na kufanyiwa baby shower.
Kuna baadhi ya watu mitandaoni walidai kwamba aliachia picha hizo baada ya kuwa tayari amejifungua.

Hata hivyo, katika kuthibisha ni kweli amejifungua, leo Jumatano Desemba 28, 2022, kwa mara ya kwanza Jokate ameachia picha yake akiwa amembeba mwanawe huyo na kumtambulisha kwa jina la Totoo nay eye ni Mama Totoo.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii zenye mamilioni ya wafuasi, Jokate ameweka picha hiyo na kuandika; “Her name is Totoo. Call me Mama Totoo…Glory to God… (Jina lake ni Totoo. Niiteni Mama Totoo…Utukufu kwa Mungu…”

Jambo hilo limewasisimua wengi wakiwemo mastaa kedekede wa Bongo ambao wameibuka na kumpongeza mno kwa hatua hiyo;

Baadhi ya mastaa hao ni pamoja na Zuchu, Sallam SK, Kajala Masanja, Esma Platnumz, Mimi Mars, Aika, Flaviana Matata, Aunt Ezekiel, MC Gara B, Gift Macha, Malika na wengine kibao.

Global TV inamtakia Totoo maisha mema akue katika afya ya mwili na roho!

Leave A Reply