The House of Favourite Newspapers

DC KINONDONI  ATOA SIRI YA NYUMBA YAKE

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Alaf (wa kwanza kulia) akimwonesha Mkuu wa Wilaya Kinondoni mabati yaliyomo katika duka hilo la maonyesho.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya uzalishaji wa mabati na vifaa vya uezekaji Alaf Ltd, Dipti Mohanty ( wa tatu kulia) akipeana mkono na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo.

 

 

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo amefunguka kuwa toka ameezeka nyumba yake kwa kutumia  mabati ya kutoka  Kampuni ya Alaf hadi sasa bado mabati hayo yanaonekana kuwa  imara.

 

Kauli hiyo aliitoa wakati wa hotuba yake ya uzinduzi wa duka jipya la maonyesho ya mabati na vifaa vingine vya uezekaji katika eneo la Mwenge-Josam House.

 

Katika hatua nyingine,  Meneja Mkuu wa Kampuni ya uzalishaji wa mabati na vifaa vya uezekaji Alaf Ltd, Dipti Mohanty, amesema kuwa duka hilo ni la pili kufunguliwa kwa kipindi cha miezi tisa hadi sasa baada ya duka la awali kuzinduliwa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.

 

Aidha, alisema kuwa duka hilo limeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia wateja juu ya ufumbuzi wa haraka wa mahitaji yao, kujifunza kuhusu bidhaa mbalimbali za Alaf,  kuweka oda za mahitaji yao ya mabati na mambo mengine.

 

 

Comments are closed.