The House of Favourite Newspapers

DC Mjema Apiga Marufuku Ibada Katikati ya Wiki, Makonda ‘Amzima’

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema,  amepiga marufuku shughuli zote za ibada zinazofanyika katikati ya juma katika wilaya yake.

 

Kufuatia agizo hilo siku za ibada zitakuwa Ijumaa kwa Waislam, Jumamosi kwa Wasabato na Jumapili kwa Wakristo wengine.

 

Amesema, kikundi chochote cha kidini kitakachofanya ibada nje ya siku hizo kitachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili. Ametaka pia wananchi kufanya ibada kwa siku zilizoelekezwa na kutumia siku nyingine kufanya kazi.

 

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametengua kauli ya Mjema ya kuzuia wananchi wa Ilala kuabudu katikati ya wiki, na ameamuru wananchi waendelee na ibada kwa kufuata utaratibu.

Comments are closed.