The House of Favourite Newspapers

DCB Yajidhatiti Kutoa Huduma Bora za Kibenki Kwa Njia za Kidigitali

0
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Nelson Swai akitoa mada kuhusu masuala ya fedha zinazovuka mipaka Kidigitali na ujumuishi wa kifedha barani Afrika jijini Dar es Salaam jana kwa baadhi ya wamiliki chipukizi wa mifumo ya Tehama wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya ufunguaji wa akaunti za benki za mtandaoni katika nchi mbalimbali na kufanya miamala kwa sarafu yoyote kwa makato madogo kwa kutumia proramu ya Grey ipatikanayo playstore na Appstore. Bwana Nelson alisema DCB imejizatiti katika matumizi ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa huduma za kibenki.
Mkurugenzi wa Uendeshaji na Tehama wa Benki ya Biashara ya DCB, Nelson Swai ( kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kutoa mada kuhusu Masuala ya fedha zinazovuka mipaka kidigitali na ujumuishi wa kifedha barani Afrika wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya ufunguaji wa  akaunti za  benki za mtandaoni katika  nchi mbalimbali  na kufanya miamala kwa sarafu yoyote kwa makato madogo kwa kutumia proramu ya Grey ipatikanayo playstore na Appstore. Kushoto kwake ni Meneja Miradi wa Ecobba, Bi. Idabente Winfried, Mkurugenzi wa laina Finance, Tonny Missokia na Mwanzilishi wa Jukwaa Afrika, Baraka Mafole. Bwana Nelson alisema DCB imejizatiti katika matumizi ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa  huduma za kibenki.
Mkurugenzi wa Uendeshaji na Tehama wa Benki ya Biashara ya DCB, Nelson Swai ( katikati) akizungumza na  baadhi ya  wamiliki chipukizi wa mifumo ya Tehama wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ufunguaji wa akaunti za benki za  mtandaoni katika nchi mbalimbaki na kufanya miamala kwa sarafu yoyote kwa makato madogo kwa kutumia proramu ya Grey ipatikanayo playstore na Appstore. Bwana Nelson alisema DCB imejizatiti katika matumizi ya teknolojia za kisasa katika utoaji wa  huduma za kibenki.
Mmoja wa wamiliki wa mifumo ya Tehama chipukizi (startup) akiuliza swali kwa Mkurugenzi  wa Uendeshaji wa Benki ya DCB, Nelson Swai (hayupo pichani) mara baada ya kutoa mada kuhusu  Masuala ya fedha.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Nelson Swai ametoa mada kuhusu masuala ya fedha zinazovuka mipaka Kidigitali na ujumuishi wa kifedha barani Afrika kwa baadhi ya wamiliki chipukizi wa mifumo ya Tehama wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya ufunguaji wa akaunti za benki za mtandaoni katika nchi mbalimbali na kufanya miamala kwa sarafu yoyote kwa makato madogo kwa kutumia proramu ya Grey ipatikanayo playstore na Appstore.
Leave A Reply