The House of Favourite Newspapers

DE GEA AWAFANYIA UMAFIA MAN UNITED, AGOMA KUSAINI

IMERIPOTIWA kuwa Kipa namba moja wa Klabu ya Manchester United, David de Gea raia wa Hispania amekataa ofa ya kusaini mkataba mpya ndani ya klabu yake hiyo kwa madai kuwa anataka kulipwa mshahara mkubwa zaidi ya Paul Pogba au sawa na Alexis Sanchez ili asaini.

De Gea ambaye analipwa £200,000 kwa wiki huku Pogba akilipwa £290,000 na Sanchez £400,000, huenda Bodi ya Uongozi ya Man U ikakaa chini na wakala wake ili kuamua hatima ya kumuongezea kiasi hicho cha fedha au la!

Aidha, kwa muda mrefu kipa huyo amekuwa akiwindwa na Real Madrid lakini United wamekuwa wagumu kumuachia kirahisi.

Comments are closed.