The House of Favourite Newspapers

DUMA: BONGO MUVI YA FAIDA INAKUJA

Daudi Michael ‘Duma’

MSANII wa filamu za Kibongo, Daudi Michael ‘Duma’ ambaye hivi karibuni amefanya uzinduzi wa filamu yake ya Nipe Changu amefunguka kuhusu sanaa ya filamu kukua ndani na nje ya nchi na waigizaji kunufaika kutokana na kazi yao.  

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Duma alisema sanaa ya Tanzania kwa sasa inakua na anaona jinsi ambavyo wasanii watanufaika.

“Niseme tu kwamba nashukuru kwa sababu mifumo inayokuja ni ya faida, siyo mifumo ya kuuziana haki miliki hivyo naamini kila msanii ambaye atafanya kazi zake vizuri, anakwenda kunufaika nazo, kikubwa ni kumuomba Mungu ili tuweze kufikia malengo,” alisema Duma.

STORI: NEEMA ADRIAN

Comments are closed.