The House of Favourite Newspapers

DEAL DONE, KICHUYA, SIMBA WAMALIZANA

Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya.

 

Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea klabu ya hiyo.

Kichuya alitakiwa kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini na tayari alimaliza mkataba na Simba. Lakini uongozi huo umefanikiwa kumalizana naye.
“Ataondoka leo kwenda Kenya kuungana na kikosi ambacho kinashiriki michuano ya SportPesa Super Cup,” kilieleza chanzo.
Kichuya ni kati ya wachezaji wamekuwa na mafanikio makubwa na kikosi cha Simba tokea watue wakitokea Mtibwa Sugar.
Kasi yake nzuri kikosini humo kwa misimu miwili mfululizo, kumemfanya kuwa kipenzi cha Wanasimba.

Comments are closed.