The House of Favourite Newspapers

Denti UDSM Aliyetuma Picha za Nyufa Mabweni ya Magufuli Adakwa na Polisi

0
Dawson.

KIJANA Kumbusho Dawson Kagine ambaye ni Mbunge katika Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) amekamatwa na Jeshi la Polisi Dar kwa kosa la kutuma picha za Hosteli za Magufuli katika chuo hicho na kupelekwa katika Kituo cha Polisi UDSM ambapo baadaye amepelekwa Police Central.

 

Kabla ya kukamatwa kwake, kiajana huyo ali-post kwenye mtandao wa Facebook hizi hapa.

Andiko la kwanza kabisa.

“Nimetoka New Hostel (Magufuli Hostel), Hosteli ambazo rais wetu amepigania mpaka zikajengwa kwa Shilingi Bilioni 10 tu za Kitanzania. Ni Ajabu sana, Huenda hizi zikawa ni hosteli zilizojengwa kwa kiwango cha chini kuliko hosteli zote barani Afrika…. Nitawaletea picha hapa siku ya kesho au ikiwezakana baadaye…… Mtatoa machozi.

Hatupo Salama…… Naomba msinipige risasi mpaka nitoe ushahidi.

NB:
Hosteli hizi zimejengwa kwa Bilioni 10 tu”

#Bilioni10Tu.

Andiko la Pili

“#JOHN_POMBE_MAGUFULI_HOSTEL.

Ikiwa ni takriban ya wiki nne tu toka hosteli hizi kuanza kukaliwa na wanafunzi, hatimaye nyufa kubwa na za kushangaza zimenza kujitokeza kwenye mojawapo ya Majengo haya alimaarufu kama JOHN POMBE MAGUFULI HOSTEL.

 

Hosteli hizi zilizinduliwa na Mh. Rais mwanzoni mwa mwaka huu na zimeanza kukaliwa Mwezi wa 11 mwaka huu. Ajabu ni kuwa nyufa zimezidi kuota kwenye mojawapo ya majengo haya. Hosteli hizi zimebeba takribani ya Wanafunzi 3840.

 

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alidai kuwa majengo haya yalijengwa kwa bilioni 10 tu za kitanzania ingawa takwimu za Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali yaani CAG waliweza kubaini kuwa majengo haya yalijengwa kwa Sh. Bilioni 54 …

 

Majengo haya kujengwa kwake yametumia miezi Sita tu kukamilika kwake.. Taarifa za awali zinadai kuwa hosteli hizi huenda zikawa ni mojawapo ya Hosteli zilizojengwa kwa kiwango cha chini kuliko Hostel zozote Barani Afrika.

Pichani ni MAGUFULI HOSTEL.
Andika #Bilioni10 Kwa kilugha chako….. Twende kazi.”

 

Moja ya picha yake akiwa na viongozi wa Chadema.

Chapisho la Tatu

MAJIBU YANGU KWA TBA.

Masaa matatu yaliyopita nilichapisha andiko langu hapa kwenye ukarasa wa Facebook nikielezea Jengo la Hostel lililojengwa kwa hisani ya Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli nikielezea kuwa yamepata nyufa.

 

Ofisa Mtendaji mkuu wa TBA bwana Elias Mwakalinga ameliambia Mwananchi kuwa anajiandaa kwenda kuangalia kama ni kweli, akaenda mbele zaidi na kusema kuwa huenda kuwa hosteli hizo ni za majengo mengine zimehusishwa na majengo mengine.

 

Nimuombe Mkurugenzi wa TBA Mh. Elias Mwakalinga kuwa sijafananisha na majengo mengine na picha hizo ni za kweli na nimepiga mwenyewe.

Nendeni Hostel Block A, nitafuteni niwasadie kuwaonyesha nyufa zilipo.

Naomba niongezee kuwa tatizo sio hilo tu, tutafutane tuwaambie na matatizo mengine.

Tunawakoa ili kuwasaidia, msituone maadui na kutafuta visingizio vingine eti majengo yatakuwa sio yenyewe….

 


Chapisho la nne

“SIO TU NYUFA BALI TBA TOLEEÑI UFAFANUZI WA MIUNDO MBINU YA MAJI MACHAFU NA BAADHI YA MAKABATI.

Jana baada ya kuchapisha Chapisho langu kupitia ukurasa wangu wa Facebook ukielezea Nyufa zilizopo kwenye mojawapo ya jengo ambalo ni Block A, TBA walifunga safari kuja kuthibitisha kama kuna nyufa kweli New Hostel.

Sio tu Nyufa bali TBA wakubali kuwa majengo haya waliyejenga Chini ya kiwangi likiwemo Block A ambalo limeanza kutoa nyufa.

Zaidi ya Nyufa lazima tukubali kuwa bado majengo haya baadhi ya miundo mbinu ni mibovu ikiwemo maji machaf hasa Mabafuni. Mabafuni hali ni mbaya sana wanafunzi wachache tu wakioga maji yanatuama na kupelekea maji machafu kuanza kutembea korodoni.

Lengo la machapisho yangu haya ni kuwasaidia TBA kuboresha na kufanya ufanisi zaidi siku za mbeleni huko watakapo pewa kazi nyingine. Hebu tuachanane na suala la miundo mbinu ya maji machafu.

 

Suala lingine ni hili (Ingawa sina uhakika kama hii ni kazi ya TBA au kuna mtu mwingine alipangiwa kazi hii) Kuhusu makabati yaliyotelekezwa takribani ya wiki 3 sasa bila kufikisiwa ukutani. Ni nini hasa chanzo ? Je mafundi wamepangiwa kazi nyingine ama?? Au ni tatizo la kifedha??. (Nendeni block

 

Nategemea TBA baadaye na hili watalifanyia kazi. Lakini suala la msingi niwapongeze TBA baada ya kuona machapisho yangu kupitia ukurasa wangu jana saaa usiku 3 usiku walifunga safari kuja Magufuli Hosteli kuangalia nyufa hizo. (Hakika mmeonyesha kuwa mnawajali wanafunzi) Heko kwenu.

 

Nategemea mtafanya marekebisho kwenye miundo mbinu ya maji pia kwani ni mibovu.
(Tembeleeni block A, na Block B)

Tukosoe kusaidia, tukusoe kwa manufaa ya Taifa.

Change ni mimi, ni wewe ni sisi….. TWAWEZA.

[​IMG]Pichani ni baadhi ya maji machafu yaliyotuama Kwenye korodi na baada ya kujaa bafuni.

[​IMG]Picha ya pili ikionyesha Makabati yaliyotelekezwa bila kufiksiwa ukutani.

CUF ya Lipumba Yamlipua Mtulia, Yaanika Figisu Zake Kabla ya Kuhamia CCM

Leave A Reply