The House of Favourite Newspapers

Dhamira ya Kujenga Uwanja Dodoma Ipo- Msigwa

0

MSEMAJI Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kuwa Serikali bado imedhamiria kujenga uwanja wa Soka katika makao makuu ya nchi Dodoma , Msigwa ameyasema hayo leo Septemba 12, jijini Dodoma wkati akitoa ripoti ya wiki ya serikali

 

“Dhamira ya kujenga uwanja wa mpira jijini Dodoma bado ipo, Serikali inakamilisha michoro ambapo mchakato huu ukikamilika, zabuni itatangazwa na ujenzi utaanza”.

 

Aidha ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imepeleka Bil. 1.5 kwenye Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili kuimarisha michezo na pia imeondoa Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye nyasi bandia ili kuimarisha miundombinu.

Leave A Reply